Jumbe 100 za Afya kwa watoto za kujifunza & kushiriki ni rahisi, na ni jumbe za kuelimisha kuhusu afya zilizoaminika na zinalenga watoto wenye umri wa miaka 8-14. Hivyo hii inajumuisha vijana wenye umri wa miaka 10-14. Tuahisi kuwa ni muhimu sana na kuna manufaa kuhakikisha kuwa vijana wenye umri wa miaka 10-14 wanafahamishwa kwa sababu kundi hili mara nyingi hutunza watoto wadogo katika familia zao. Pia ni muhimu kutambua na kupongeza kazi wanayoifanya ili kusaidia familia zao kwa njia hii.

Ujumbe 100 unajumuisha jumbe 10 katika kila mojawapo ya mada muhimu ya afya: Malaria, Kuhara, Lishe bora, mafua na kukohoa, Minyoo, Maji na Usafi, Uchanjaji, Ukimwi, Ajali na Majeraha, Maendeleo ya Mapema ya Watoto. Ujumbe wa afya uliorahisishwa unalenga wazazi, waalimu wa afya ili kutumia kwa watoto nyumbani, shuleni, katika vilabu na kliniki.

Hizi ni jumbe 10 katika mada ya 1: KUTUNZA WATOTO

 1. Cheza michezo, kumbatia, zungumza, cheka na imba na watoto wachanga na watoto wadogo uwezavyo.
 2. Wototo wachanga na wadogo hukasirika, huogopa na hulia kwa urahisi na hawawezi kuelezea hisia zao. Daima kuwa na fadhili.
 3. Watoto wadogo hujifunza haraka: jinsi ya kutembea, kutoa sauti, kula na kunywa. Wasaidie na pia waruhusu wafanye makosa salama pia!
 4. Wasichana wote na wavulana wote ni muhumu sawa. Tendea kila mmoja vyema, haswa watoto walio wagonjwa au walio na ulemavu.
 5. Watoto wadogo huiga matendo ya wale walio karibu nao. Kuwa mwangalifu, kuwa na nidhamu ukiwa karibu na wao na uwaonyeshe njia sahihi.
 6. Wakati watoto wadogo wanapolia, kuna sababu (njaa, woga au uchungu). Jaribu ujue ni kwa nini.
 7. Saidia katika kutayarisha watoto wadogo kusoma katika shule kwa kucheza michezo ya nambari na maneno, kupaka rangi na kuchora. Waambie hadithi, imba nyimbo na ucheze.
 8. Katika kikundi, tanzama na urekodi katika kijitabu jinsi mtoto mchanga hukua na wakati huanza mambo muhimu ya kwanza kama vile kutamka, kutembea na kuongea.
 9. Saidia katika kuzuia magonjwa kwa kuwasaidia watunzaji watoto walio wazima na watoto wakubwa kuangalia ikiwa watoto wachanga na wadogo ni safi (haswa mikono na nyuso), wanakunywa maji safi na wanakula chakula kizuri na cha kutosha.
 10. Tunza watoto wachanga na wadogo kwa upendo lakini usijisahau. Wewe ni wa maana pia.

Jumbe hizi za afya zimeangaliwa na wataalamu wa elimu ya afya na wataalamu wa afya na pia zinaweza kupatikana kwenye tovuti ya ORB: http://www.health-orb.org.

Hii ni baadhi ya mifano ya mazoezi ambayo yatasaidida watoto kuelewa zaidi kuhusu mada na kushiriki ujumbe na wenzao.

Kutunza watoto: Watoto wanaweza kufanya nini?

 • Tengeneza ujumbe wetu kuhusu Kutunza Watoto kwa kutumia maneno yetu wenyewe katika lugha yetu wenyewe!
 • Kariri jumbe ili tusisahau!
 • Shiriki jumbe hizi na watoto wengine na familia zetu!
 • Gawa vikundi vya wasichana na wavulana; wavulana wacheze ‘michezo ya wasichana’ na wasichana wacheze ‘michezo ya wavulana’. Baadaye, makundi yote mawili yajadili kuhusu michezo hio. Kwa mfano, mnakubali michezo ikiitwa michezo ya wavulana au wasichana? Kwa nini au kwa nini sivyo?
 • Jadili tabia ‘nzuri’ au ‘mbaya’ katika shule au nyumbani na kwa nini inaelezewa hivyo.
 • Tengeneza mabango ya kuwaonyesha wengine tunachofahamu kuhusu mada hii.
 • Andaa mashindano ya kutengeneza vitu vya kuchezea kama vile simu, kayamba, matofali, mwanasesere, wanyama, vitabu vya picha – nyumbani, shuleni na katika makundi ya jamii.
 • Tengeneza michoro na mabango ya kuonyesha hatua rahisi za kuzuia magonjwa kama vile kunawa mikono kwa kutumia sabuni, uchanjaji na kula chakula bora.
 • Tengeneza mchezo wa kuigiza mfupi kuhusu watunzaji wanaocheza na watoto wadogo. Wanaweza kuigiza mazungumzo kati ya akina mama wawili; mmoja anayeamini kuwa watoto wadogo wanafaa kunyamazishwa na mwingine anayeamini watoto wadogo wanafaa kujifurahisha! Iga / fanya hisia / hisia tu pamoja na ishara na maneno ya uso. Watoto wale wengine wabahatishe hisia hizo zinahusu nini.
 • Uliza wazazi na akina nyanya na babu ni kwa nini na ni nini huwafanya watoto wachanga walie au wacheke kisha shiriki matokeo utakayopata darasani.
 • Darasa au kikundi wanaweza kupanga mtoto mchanga kutoka katika jamii mtaani. Mama atatembelea kikundi hiki kila mwezi ili kushiriki jinsi mtoto anavyokua.
 • Tengeneza wimbo ili kuelezea hatua rahisi za kuzuia magonjwa kama vile kuhakikisha usafi na maji safi ya kunywa, imba hizo nyimbo nyumbani pamoja na ndugu zako wadogo.
 • Watoto wakubwa wawahoji wazazi na kuuliza nini kilikuwa ngumu kwao wakati wa kuwatunza watoto wachanga na watoto wadogo, na nini kiliwasaidia zaidi.
 • Uliza mfanyakazi wa afya au mwalimu wa sayansi kukuambia zaidi kuhusu jinsi ubongo wa mtoto mchanga hukua.
 • Watoto wakubwa wanaweza kuuliza wazee katika jamii kuwafundisha nyimbo, hadithi na michezo, na kuimba nyimbo za watoto wachanga na watoto wadogo.
 • Watoto wanaweza kuwauliza watu wazima ni nini wanachofikiria ni muhimu kufanya ili kuzuia watoto wachanga dhidi ya maambukizi ya magonjwa.

Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na www.childrenforhealth.org au clare@childrenforhealth.org
.

Swahili Home