Jumbe 100 za Afya kwa watoto za kujifunza & kushiriki ni rahisi, na ni jumbe za kuelimisha kuhusu afya zilizoaminika na zinalenga watoto wenye umri wa miaka 8-14. Hivyo hii inajumuisha vijana wenye umri wa miaka 10-14. Tuahisi kuwa ni muhimu sana na kuna manufaa kuhakikisha kuwa vijana wenye umri wa miaka 10-14 wanafahamishwa kwa sababu kundi hili mara nyingi hutunza watoto wadogo katika familia zao. Pia ni muhimu kutambua na kupongeza kazi wanayoifanya ili kusaidia familia zao kwa njia hii.

Ujumbe 100 unajumuisha jumbe 10 katika kila mojawapo ya mada muhimu ya afya: Malaria, Kuhara, Lishe bora, mafua na kukohoa, Minyoo, Maji na Usafi, Uchanjaji, Ukimwi, Ajali na Majeraha, Maendeleo ya Mapema ya Watoto. Ujumbe wa afya uliorahisishwa unalenga wazazi, waalimu wa afya ili kutumia kwa watoto nyumbani, shuleni, katika vilabu na kliniki.

Hizi ni jumbe 10 kwa mada ya 10: UKIMWI

 1. Mwili wetu ni wa ajabu na kila siku unatumia njia za kipekee kutukinga dhidi ya magonjwa kupitia kwa vijududu tunavyopumua, kula, kunywa au kugusa.
 2. HIV ni kiini kiitwacho virusi. (Herufi V inaashiria Virusi). Ni virusi hatari zaidi ambavyo huzuia mwili wetu kujilinda kutokana kwa viini vingine.
 3. Wanasayansi wametengeneza madawa ambayo yanazuia HIV kuwa hatari lakini hakuna mtu aliyepata njia ya kuiondoa kabisa kutoka mwilini.
 4. Baada ya muda na bila dawa, watu wenye HIV hupata UKIMWI. UKIMWI ni jumla ya magonjwa yanayodhoofisha mwili.
 5. Virusi vya HIV haviwezi kuonekana na huishi kwenye damu na vioevu vingine vinayotengenezwa na mwili wakati wa ngono. HIV inaweza kusambazwa (1) wakati wa ngono, (2) kutoka kwa mama walioambukizwa hadi kwa watoto wachanga na (3) katika damu.
 6. Watu hujilinda dhidi ya HIV kupitia ngono kwa (1) kususia ngono, (2) kuwa mwaminifu katika uhusiano au (3) kufanya ngono kwa kutumia kondomu (ngono salama).
 7. Unaweza kucheza, kula na kunywa pamoja, kushikana mikono na watu walio na virusi vya HIV na ukimwi. Matendo haya ni salama na huwezi kupata virusi kwa njia hii.
 8. Watu walio na ukimwi wakati mwingine huhisi woga na huzuni. Kama kila mtu, wanahitaji upendo na msaada, hii ni hata familia zao. Wanahitaji kuzungumza kuhusu wasiwasi wao.
 9. Ili kujisaidia na kusaidia wengine, watu wanaodhani kuwa wana HIV au ukimwi lazima waende kwenye kliniki au hospitali kufanyiwa uchunguzi na ushauri.
 10. Katika nchi nyingi, watu ambao wana HIV wanapata msaada na matibabu. Dawa inayoitwa antiretroviral therapy (ART) huwasaidia kuishi maisha marefu.

Jumbe hizi za afya zimeangaliwa na wataalamu wa elimu ya afya na wataalamu wa afya na pia zinaweza kupatikana kwenye tovuti ya ORB: http://www.health-orb.org.

Hii ni baadhi ya mifano ya mazoezi ambayo yatasaidida watoto kuelewa zaidi kuhusu mada na kushiriki ujumbe na wenzao.

HIV na UKIMWI: Watoto wanaweza kufanya nini?

 • TENGENEZA ujumbe kuhusu HIV na UKIMWI kwa kutumia maneno yetu wenyewe katika lugha yetu wenyewe!
 • KARIRI jumbe ili tusisahau!
 • SHIRIKI ujumbe pamoja na watoto wengine na familia zetu!
 • KUSANYA vipeperushi na maelezo kuhusu HIV na UKIMWI na kuwaeleza wengine katika jamii.
 • ALIKA mhudumu wa afya katika shule yetu ili aweze kujibu maswali kuhusu HIV na UKIMWI.
 • TAFUTA njia za kuwasaidia watoto katika jamii yetu ambao wanaathiriwa na ukimwi.
 • CHEZA mchezo wa Lifeline ili kutambua tabia ambazo zinaweza kutuweka kwenye hatari ya maambukizi ya HIV.
 • BUNI na IGIZA mchezo wa Sahihi au LA kuhusu jinsi virusi vya HIV husambazwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Tumia ULIZAmaswali mwishoni ili kusaidika.
 • JIFUNZE kuhusu mbinu zitakazotusaidia kuongea kuhusu urafiki maalum na hisia zetu za kingono.
 • CHEZA mchezo wa Fleet of Hopeili ujue ni tabia zipi ambazo ni salama na tutazichagua kujikinga dhidi ya HIV katika urafiki wetu maalum.
 • FIKIRI kuhusu ugumu ambao mtu aliye na HIV na UKIMWI hupitia na tunachoweza kufanya ili kuwasaidia.
 • IGIZA kuwa na virusi vya HIV na jinsi inavyoweza kuwa ukiwa na HIV.
 • SKIZA na ujadili hadithi kuhusu watu wanaoishi na HIV na shidi zinazowakumba.
 • FANYA jaribio la kujua kile tunachokijua kuhusu HIV na UKIMWI.
 • TENGEZA kisanduku cha maswali katika darasa letu kwa maswali yetu kuhusu HIV na UKIMWI.
 • TENGEZA bango la shule yetu kuhusu HIV na UKIMWI.
 • IGIZA mchezo kuhusu msichana aitwaye Meena au mvulana aitwaye Rajeev na mamake aliye na HIV na jinsi Meena anamshawishi mamake kwenda kwenye kliniki kupata dawa za ART (anti-retroviral therapy).
 • BUNI klabu ya HIV na UKIMWI ili kupatiana ufahamu shuleni na katika familia.
 • ULIZA mfumo wetu wa kinga hufanya kazi vipi? Ni chakula kipi kinachosaidia mfumo wetu wa kinga mwilini kuwa na nguvu na tayari kutukinga? Je, HIV ni nini na UKIMWI ni nini? Herufi hizo zinasimama nini? Ni nini kinachotokea wakati mtu anajua ana HIV? Ni nini kinachotokea wakati mtu anapopata UKIMWI? HIV husambazwa vipi kutoka kwa binadamu mmoja hadi mwingine? Ni vipi haisambazwi? Tunawezaje kujilinda dhidi yake? Je! Watu hupimwa na kutibiwa vipi dhidi ya HIV? Dawa zinawezaje kupunguza hatari ya kusambaza virusi kutoka kwa mama hadi kwa mtoto? Je! ART (anti-retroviral therapy) hufanya kazi vipi na ni wakati mgani ambao mtu anapaswa kuzitumia? Ni vipi na wakati gani ambapo urafiki hugeuka kuwa wa kimapenzi? Mtu hutumiaje kondomu kwa usahihi? (Kiume/kike) Ni njia gani bora za kuwasaidia marafiki na jamaa ambao wanaishi na virusi vya HIV ili wawe na afya? Kliniki iliyopo karibu zaidi inayowasaidia wagonjwa wa HIV na ukimwi iko wapi?

Kwa maelezo zaidi maalum kuhusuMchezo wa Lifeline au mchezo wa Fleet of Hope au mfano wa Mchezo wa True or False, au maelezo mengine yoyote tafadhali wasiliana na www.childrenforhealth.org au clare@childrenforhealth.org
.

Swahili Home