Jumbe 100 za Afya kwa watoto za kujifunza & kushiriki ni rahisi, na ni jumbe za kuelimisha kuhusu afya zilizoaminika na zinalenga watoto wenye umri wa miaka 8-14. Hivyo hii inajumuisha vijana wenye umri wa miaka 10-14. Tuahisi kuwa ni muhimu sana na kuna manufaa kuhakikisha kuwa vijana wenye umri wa miaka 10-14 wanafahamishwa kwa sababu kundi hili mara nyingi hutunza watoto wadogo katika familia zao. Pia ni muhimu kutambua na kupongeza kazi wanayoifanya ili kusaidia familia zao kwa njia hii.

Ujumbe 100 unajumuisha jumbe 10 katika kila mojawapo ya mada muhimu ya afya: Malaria, Kuhara, Lishe bora, mafua na kukohoa, Minyoo, Maji na Usafi, Uchanjaji, Ukimwi, Ajali na Majeraha, Maendeleo ya Mapema ya Watoto. Ujumbe wa afya uliorahisishwa unalenga wazazi, waalimu wa afya ili kutumia kwa watoto nyumbani, shuleni, katika vilabu na kliniki.

Hizi ni jumbe 10 kwa mada ya 2: Kikohozi, mafua na ugonjwa

 1. Moshi kutoka kwenye moto wa kupika una vitu vidogo ndani yake ambayo vinaweza kuingia kwenye mapafu na kusababisha ugonjwa. Epuka moshi kwa kupikia nje au mahali hewa safi inaweza kuingia na moshi kutoka.sa,, picture of a person coughing
 2. Kuvuta sigara hufanya mapafu dhaifu. Kupumua moshi kutoka kwa watu wanaovuta sigari ina madhara pia.
 3. Kila mtu hupatwa na kikohozi na mafua. Watu wengi hupata nafuu haraka. Ikiwa kikohozi au mafua imechukua zaidi ya wiki tatu, enda kwenye kliniki cha afya.
 4. Kuna aina ya viini vinavyoitwa bakteria na vingine vinavyoitwa virusi. Virusi husababisha kikohozi na mafua na vinaweza kuuawa kwa kutumia dawa.
 5. Mapafu ni sehemu ya mwili inayopumua. Kikohozi na mafua hufanya mapafu kuwa dhaifu. Neumonia ni kiini cha bakteria ambacho husababisha ugonjwa mbaya katika mapafu dhaifu.
 6. Dalili ya neumonia (ugonjwa mbaya) ni kupumua kwa haraka. Skiza hali ya kupumua. Angalia kifua kinavyopanda na kushuka. Dalili zingine ni homa, ugonjwa na maumivu ya kifua.
 7. Mtoto mchanga aliye na umri wa chini ya miaka miwili na anayepumua mara 60 kwa dakika au zaidi anafaa kupelekwa kwa mfanyakazi wa afya HARAKA! Kupumua haraka kwa watoto walio na umri wa miaka 1-5 kuko zaidi ya pumzi 20-30 kwa kila dakika.
 8. Chakula bora (na kunyonyesha watoto wachanga), nyumbani pasipo na moshi na uchanjaji husaidia kuzuia magonjwa makali kama vile neumonia.
 9. Tibu kikohozi au mafua kwa kujiweka katika hali joto, kunywa vinywaji tamu mara kwa mara (kama vile supu na jusi), kupumzika na kuhakikisha mapua yako ni safi.
 10. Komesha kikohozi, mafua na magonjwa mengine kutoenea kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Hakikisha mikono na vyombo vya chakula na maji ni safi, tumia karatasi wakati unakohoa.

Jumbe hizi za afya zimeangaliwa na wataalamu wa elimu ya afya na wataalamu wa afya na pia zinaweza kupatikana kwenye tovuti ya ORB: http://www.health-orb.org.

Hii ni baadhi ya mifano ya mazoezi ambayo yatasaidida watoto kuelewa zaidi kuhusu mada na kushiriki ujumbe na wenzao.

Kikohozi, mafua & magonjwa: Watoto wanaweza kufanya nini?

 • Tengeneza ujumbe wetu kuhusu Kikohozi, Mafua & Ugonjwa kwa maneno yetu wenyewe na lugha yetu wenyewe!
 • Kariri jumbe ili tusisahau!
 • SHIRIKI jumbe hizi na watoto wengine na familia zetu! Fanya mpango wa nyumba yako. Ni wapi kuna moshi, ni wapi hakuna? Ni wapi kwa kuchezea ambapo ni salama kwa watoto mbali na moshi?.
 • Tengeneza bango ili kuwahimiza wazazi kuwapeleka watoto wao kupewa chanjo dhidi ya maradhi hatari kama vile ukambi na kifaduro.
 • Tengeneza wimbo kuhusu neumonia na kushiriki na familia zetu na marafiki.
 • Tengeneza timazi iliyo na kamba na jiwe ili kutusaidia kuhesabu wakati kupumua ni haraka na wakati kupumua ni kwa kawaida, na kuonyesha yale tuliyojifunza kwa familia zetu.
 • Tengeneza mchezo wetu wa kuigiza kuhusu kunyonyesha watoto wachanga.
 • Fanya mcheza wa kuigiza kuhusu kuhakikisha kuna baridi wakati wa homa na joto wakati wa mafua.
 • Weka mfereji wa nyumbani na shuleni ili kutusaidia kunawa mikono kwa kutumia sabuni kabla ya kula au baada ya kwenda msalani.
 • Jifunze jinsi ya kuosha mikono kwa kutumia sabuni na maji ili kukomesha viini kuenea, na kujilinda binafsi dhidi ya kikohozi na mafua.
 • Fanya jaribio kuhusu maarifa yetu ya neumonia kwa kuigiza matukio tofauti ambayo yanaweza kuwa neumonia au yanaweza kuwa mafua.
 • ULIZA ni nini dalili hatari za neumonia? Shiriki tunachojifunza pamoja na jamii zetu.
 • ULIZA ni wapi uvutaji sigara ni marufuku? Shule yenu ni marufuku kwa uvutaji wa sigara?
 • ULIZA ni nini hutufanya kupumua haraka?
 • Tunaweza kupima kupumua kwetu ili kujifunza kutambua kupumua haraka wakati mtu ako hatarini kutokana na neumonia.
 • ULIZA ni njia gani mpya na za zamani za kutibu kikohozi na mafua?
 • ULIza jinsi viini huenea? Jifunze kwa kuchezamchezo wa kupeana mkono.

Kwa maelezo zaidi kuhusu mfereji, timazi au mchezo wa kupeana mkono, au maelezo mengine yoyote, tafadhali wasiliana na www.childrenforhealth.org au clare@childrenforhealth.org.

Swahili Home