Jumbe 100 za Afya kwa watoto za kujifunza & kushiriki ni rahisi, na ni jumbe za kuelimisha kuhusu afya zilizoaminika na zinalenga watoto wenye umri wa miaka 8-14. Hivyo hii inajumuisha vijana wenye umri wa miaka 10-14. Tuahisi kuwa ni muhimu sana na kuna manufaa kuhakikisha kuwa vijana wenye umri wa miaka 10-14 wanafahamishwa kwa sababu kundi hili mara nyingi hutunza watoto wadogo katika familia zao. Pia ni muhimu kutambua na kupongeza kazi wanayoifanya ili kusaidia familia zao kwa njia hii.

Ujumbe 100 unajumuisha jumbe 10 katika kila mojawapo ya mada muhimu ya afya: Malaria, Kuhara, Lishe bora, mafua na kukohoa, Minyoo, Maji na Usafi, Uchanjaji, Ukimwi, Ajali na Majeraha, Maendeleo ya Mapema ya Watoto. Ujumbe wa afya uliorahisishwa unalenga wazazi, waalimu wa afya ili kutumia kwa watoto nyumbani, shuleni, katika vilabu na kliniki.

Hizi ni jumbe 10 katika mada ya 3: Uchanjaji

 1. Mamilioni ya wazazi ulimwenguni pote kila mwaka huhakikisha watoto wao wamekua na kuwa na nguvu na wamekingwa kutokana na magonjwa kwa kupewa chanjo.
 2. Wakati uko mgonjwa na umepatwa na maradhi ambukizi, kiini kidogo na kisichoonekana kimeingia kwenye mwili wako. Kiini hiki huzaa viini wengi na hufanya mwili wako kutofanya kazi vizuri.
 3. Mwili wako uko na walinzi maalumu wanaoitwa kingamwili na ambao hupigana na viini. Wakati viini vimeuawa, kingamwili hubaki kwenye mwili ikiwa tayari kupigana tena.
 4. Uchanjaji huweka antijeni kwenye mwili wako (kupitia kudungwa sindano au kwa mdomo) Hufunza mwili wako kutengeneza kingamwili walinzi ili kupigana na magonjwa.
 5. Baadhi ya chanjo hupaswa kupeanwa zaidi ya mara moja ili kusaidia mwili kujenga antibodi ili kuzuia ugonjwa.
 6. Magonjwa ya kutisha yanayosababisha kifo na mateso, kama surua, kifua kikuu, diphtheria, kikohozi kinachochochea, polio na tetanasi (na zaidi!), yanaweza kuzuiliwa na chanjo.
 7. Ili kukinga mwili wako, unapaswa kuchanjwa kabla ya ugonjwa kuzuka.
 8. Ili kuwakinga watoto, chanjo hutolewa kwa watoto wachanga mara moja. Ikiwa mtoto mchanga atakosa kuchanjwa wakati huu, anaweza kuchanjwa baadaye.
 9. Watoto wanaweza kuchanjwa wakati tofauti dhidi ya magonjwa tofauti. Tambua wakati na mahali ambapo jamii yako huwachanja watoto.
 10. Ikiwa watoto wachanga hawajihisi vyema katika siku ya uchanjaji, bado wanaweza kupata chanjo hiyo.

Jumbe hizi za afya zimeangaliwa na wataalamu wa elimu ya afya na wataalamu wa afya na pia zinaweza kupatikana kwenye tovuti ya ORB: http://www.health-orb.org.

Hii ni baadhi ya mifano ya mazoezi ambayo yatasaidida watoto kuelewa zaidi kuhusu mada na kushiriki ujumbe na wenzao.

Uchanjaji: watoto wanaweza kufanya nini?

 • TENGENEZA jumbe kuhusu UCHANJAJI kwa kutumia maneno yetu wenyewe na katika lugha yetu wenyewe!
 • KARIRI jumbe ili tusisahau!
 • SHIRIKI jumbe hizi na watoto wengine na familia zetu!
 • TENGENEZA mabango ya siku za uchanjaji na uyaweke mahali ambapo kila mtu anaona.
 • TENGENEZA mchezo wa kuigiza kuhusu jinsi ya kukomesha magonjwa yanayosababisha kifo yanayowasumbua watoto katika kijiji chenu.
 • TENGENEZA hadithi kwa kutumia picha ya chanjo bingwa zinazopigana na magonjwa hatari ili kutukinga.
 • TENGENEZA BANGO ya ugonjwa mmoja au zaidi unaoweza kuzuiwa na chanjo kama Diphtheria, Surua na Rubella, Pertusisi, kifua kikuu, Tetenasi & Polio
 • TENGENEZA mchezo wa kuigiza au hadithi kuhusu Mwili wa Aunty, mlizi wa aina yake aliye na nguvu ya kutuweka salama na vyema.
 • JIFUNZE kuhusu magonjwa yote na uwaeleze watoto wengine na familia zetu kile tunachojifunza!
 • TENGENEZA Kadi maalum ya siku ya kuzaliwa kwa mtoto mzaliwa na mama yake ikiwa na nyakati za mtoto kupata chanjo na uwatakie furaha na afya katika mwaka wao wa kwanza wa maisha!
 • JUA zaidi kuhusu magonjwa mengi ambayo sisi hujikinga kwa kutumia chanjo.
 • JUA zaidi ya jinsi ya kuwasaidia watoto wenye ulemavu.
 • TENGENEZA MASWALI NA UYAJIBU ili kutambua kile tunachojua kuhusu chanjo. Shiriki na marafiki na familia.
 • JUA ni chanjo zipi tunahitaji zaidi ya mara moja. Na usaidie KUTAFUTA watoto ambao hawakupata chanjo.
 • TAMBUA NGUVU MAALUM ya magonjwa na jinsi chanjo husishinda nguvu hizi.
 • ANGALIA kila mtu katika darasa letu na Waalimu ikiwa wamepata chanjo zao zote.
 • TAMBUA kama kuna hafla maalum za chanjo ama siku na majuma ya afya ambapo watoto wote na watoto wachanga wanaweza kuenda kupata chanjo.
 • TAMBUA ikiwa kuna mtu katika familia yangu amekosa kupata chanjo ili aweze kuipata.
 • ULIZA kuhusu chanjo katika nchi yangu na ni LINI tunaweza kuchanjwa.
 • TAMBUA ikiwa kuna mtu yeyote katika familia alipata mojawapo ya magonjwa hatari na ni nini kilitokea.

Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na www.childrenforhealth.org au clare@childrenforhealth.org
.

Swahili Home