Jumbe 100 za Afya kwa watoto za kujifunza & kushiriki ni rahisi, na ni jumbe za kuelimisha kuhusu afya zilizoaminika na zinalenga watoto wenye umri wa miaka 8-14. Hivyo hii inajumuisha vijana wenye umri wa miaka 10-14. Tuahisi kuwa ni muhimu sana na kuna manufaa kuhakikisha kuwa vijana wenye umri wa miaka 10-14 wanafahamishwa kwa sababu kundi hili mara nyingi hutunza watoto wadogo katika familia zao. Pia ni muhimu kutambua na kupongeza kazi wanayoifanya ili kusaidia familia zao kwa njia hii.

Ujumbe 100 unajumuisha jumbe 10 katika kila mojawapo ya mada muhimu ya afya: Malaria, Kuhara, Lishe bora, mafua na kukohoa, Minyoo, Maji na Usafi, Uchanjaji, Ukimwi, Ajali na Majeraha, Maendeleo ya Mapema ya Watoto. Ujumbe wa afya uliorahisishwa unalenga wazazi, waalimu wa afya ili kutumia kwa watoto nyumbani, shuleni, katika vilabu na kliniki.

Hizi ni jumbe 10 kuhusu mada ya 4: MALARIA

 1. Malaria ni ugonjwa unaoenezwa unapoumwa na mbu aliyeambukizwa.
 2. Malaria ni ugonjwa hatari. Malaria husababisha homa na hata kifo hasa kwa watoto na wanawake wajawazito.
 3. Jikinge dhidi ya malaria kwa kulala ndani ya neti iliyotibiwa inayoweza kuua mbu na kuwazuia kuuma.
 4. Mbu wanaoeneza malaria kwa kawaida huuma kati ya jua kutua na jua kuchomoza.
 5. Watoto wanapopata malaria wanaweza kukua na kukuza polepole zaidi.
 6. Kuna aina tatu ya kunyunyiza kiuawadudu ili kuua mbu wanaosababisha malaria: kunyunyiza dawa ndani ya nyumba, kunyunyiza dawa hewani na kwenye maji.
 7. Ishara za malaria ni homa ya kali, maumivu ya kichwa, maumivu ya misuli na tumbo na kutetemeka. Vipimo vya dharura na matibabu huokoa maisha.
 8. Malaria inaweza kuzuiliwa na kutibiwa kwa dawa kama inavyoashiriwa na mhudumu wa afya.
 9. Malaria huishi kwenye damu ya mtu aliyeambukizwa na huweza kusababisha anemia, inayomfanya mtu kuhisi uchovu na unyonge.
 10. Dawa dhidi ya malaria zinaweza kuzuia na kupunguza malaria na anemia katika sehemu na wakati ambapo kuna malaria kwa wingi katika jamii.

Jumbe hizi za afya zimeangaliwa na wataalamu wa elimu ya afya na wataalamu wa afya na pia zinaweza kupatikana kwenye tovuti ya ORB: http://www.health-orb.org.

Hii ni baadhi ya mifano ya mazoezi ambayo yatasaidida watoto kuelewa zaidi kuhusu mada na kushiriki ujumbe na wenzao.

MALARIA: Watoto wanaweza kufanya nini?

 • TENGENEZA jumbe zetu zinazohusu MALARIA kwa kutumia maneno yetu na katika lugha yetu.
 • KARIRI jumbe ili tusisahau!
 • SHIRIKI jumbe hizi na watoto wengine na familia zetu!
 • TENGENEZA bango ili kuonyesha wengine jinsi malaria huenea na jinsi tunaweza kujiunga na vita ili kuzuia malaria!
 • BUNI hadithi au michezo ya kuigiza kuhusu mzunguko wa maisha ya mbu na uwaambie au kuwaonyesha watoto wengine!
 • TENGENEZA mabango ya kuonyesha jinsi ya kutumia na kutunza neti zilizotibiwa kwa kutumia kiuwa wadudu.
 • ELEZA hadithi na utengeneze mabango ili kuonyesha wengine jinsi ya kuzuia kuumwa na mbu.
 • BUNI hadithi au michezo ya kuigiza inayoonyesha jinsi mtoto mmoja hutambua ishara za malaria katika mtoto mwingine na kuwauliza watu wazima kumpeleka mtoto huyo kupimwa.
 • BUNI hadithi au mchezo wa kuigiza kuhusu ishara za malaria na anemia, jinsi minyoo husababisha anemia na jinsi malaria inasababisha kupungua kwa damu.
 • TENGENEZA mabango kuhusu vyakula vyenye virutubishi vya aina ya ayoni katika jamii yenu.
 • WASAIDIE watoto wadogo kukaa ndani ya neti wakati mbu wanauma!
 • Hakikisha neti za kitanda zimewekwa ndani ya vitanda vizuri na hazina mashimo!
 • BUNI hadithi au michezo ya kuigiza kuhusu sababu zinazowafanya watu kutopenda neti za kitandani na kile wanachoamini neti hizi hufanya na kile hazifanyi!
 • PANGA kampeni ya kuonyesha watu jinsi ya kutumia neti za kitandani!
 • MKARIBISHE mhudumu wa afya kutembelea shule yenu na kuwaelezea watoto wakubwa kuhusu neti za kitandani na vipimo!
 • TUMIA wimbo, ngoma na michezo ya kuigiza ili kushiriki jumbe hizi na wengine!
 • ULIZA ni watu wangapi katika familia yetu wamekuwa na malaria? Jinsi tunavyoweza kuzuia malaria Jinsi na wakati wa kuweka neti za kitandani zilizotibiwa ili kutumia kuua wadudu na kutumia skrini za dirisha na jinsi zinafanya kazi. Je, watu wanaweza kupata wapi neti zilizotibiwa ili kuzitumia kuua wadudu katika jamii? Je, malaria huua aje? Kwa nini hasa malaria ni hatari kwa wanawake wajawazito na watoto? Je, wahudumu wa afya huwapa nini wanawake walio na watoto kuwazuia kupata malaria na wao huipata wakati gani? Je, ayoni na vyakula vyenye virutubishi vingi vya ayoni (nyama, nafaka na mboga za kijani) husaidia aje katika kuzuia anemia? Watu wanaweza kujikinga na kuwakinga wengine aje kutokana na kuumwa na mbu? Je, vipimo maalum vya kuangalia ikiwa kuna malaria kwenye damu huitwaje?

Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na www.childrenforhealth.org au clare@childrenforhealth.org
.

Swahili Home