Jumbe 100 za Afya kwa watoto za kujifunza & kushiriki ni rahisi, na ni jumbe za kuelimisha kuhusu afya zilizoaminika na zinalenga watoto wenye umri wa miaka 8-14. Hivyo hii inajumuisha vijana wenye umri wa miaka 10-14. Tuahisi kuwa ni muhimu sana na kuna manufaa kuhakikisha kuwa vijana wenye umri wa miaka 10-14 wanafahamishwa kwa sababu kundi hili mara nyingi hutunza watoto wadogo katika familia zao. Pia ni muhimu kutambua na kupongeza kazi wanayoifanya ili kusaidia familia zao kwa njia hii.

Ujumbe 100 unajumuisha jumbe 10 katika kila mojawapo ya mada muhimu ya afya: Malaria, Kuhara, Lishe bora, mafua na kukohoa, Minyoo, Maji na Usafi, Uchanjaji, Ukimwi, Ajali na Majeraha, Maendeleo ya Mapema ya Watoto. Ujumbe wa afya uliorahisishwa unalenga wazazi, waalimu wa afya ili kutumia kwa watoto nyumbani, shuleni, katika vilabu na kliniki.

Hizi ni jumbe 10 kuhusu mada ya 5: KUHARA

 1. Kuharisha ni pale mtu anapotoa kinyesi chenye umyevunyevu kinachotokea mara tatu au zaidi kwa siku.
 2. Kuharisha husababishwa na vijidudu kuingia kwenye kinywa kutokana na chakula au kinywaji kilichochafuliwa, au kugusa kinywa kwa vidole chafu au kutumia vijiko au vikombe chafu.
 3. Kupoteza maji na chumvi (iliyo kwenye viowevu) hufanya mwili kuwa dhaifu. Ikiwa viowevu havitarudishwa mwilini, watoto wachanga wanaweza kufa wanapoharisha kwa haraka kutokana na ukosefu wa maji mwilini.
 4. Kuharisha kunaweza kuzuiliwa kwa kumpa mtu vinywaji safi kama vile maji safi au nazi au maji ya mchele. Watoto wadogo wanahitaji maziwa ya mama zaidi ya yote.
 5. Mtoto anayeharisha anaweza kuwa na kinywa kilichokauka na ulimi, macho yaliyobonyea ndani, kukosa machozi na mikono na miguu yenye baridi. Watoto wachanga pia wanaweza kuwa na sehemu laini iliyobonyea ndani kwenye kichwa.
 6. Watoto wanaopata kinyesi chenye unyevunyevu zaidi ya mara tano kwa siku au damu kwenye kinyesi au hata wanaoanza kutapika pia NI LAZIMA wapelekwe kwa mhudumu wa afya.
 7. ORS ni mchanganyiko wa chumvi za kurudisha viowevu mwilini. Unaweza kupata ORS kwenye kliniki na maduka. Changanya jinsi inavyofaa kwa kutumia maji safi ili kutengeneza kinywaji bora zaidi cha wakati mtu anaharisha.
 8. Dawa nyingi za kuharisha hazifanyi kazi lakini dawa za zinki hukomesha kuharisha haraka zaidi kwa watoto wenye zaidi ya miezi 6. Pia, vinywaji vya ORS NI LAZIMA apewe anayeharisha.
 9. Watoto wadogo wanaoharisha huhitaji chakula kitamu kilichibondwabondwa mara nyingi iwezekanavyo ili kuimarisha miili yao.
 10. Unaweza kuzuia kuharisha kwa watoto wachanga kwa kuwanyonyesha, kuhakiksha mitindo mizuri ya usafi, uchanjaji (hasa dhidi ya virusi vya rota na surua) na kuhakikisha chakula ni salama.

Jumbe hizi za afya zimeangaliwa na wataalamu wa elimu ya afya na wataalamu wa afya na pia zinaweza kupatikana kwenye tovuti ya ORB: http://www.health-orb.org.

Hii ni baadhi ya mifano ya mazoezi ambayo yatasaidida watoto kuelewa zaidi kuhusu mada na kushiriki ujumbe na wenzao.

KUHARA: Watoto wanaweza kufanya nini?

 • TENGENEZA jumbe zetu zinazohusu KUHARA kwa kutumia maneno yetu wenyewe katika lugha yetu wenyewe!
 • KARIRI jumbe ili tusisahau!
 • SHIRIKI jumbe hizi na watoto wengine na familia zetu!
 • TENGENEZA Mtego rahisi wa nzi ili kuzuia nzi wanaobeba viini kugusa chakula.
 • TENGENEZA bango ili kuwaonyesha wengine ishara hatari za kuharisha.
 • BUNI mchezo mfupi kuhusu wakati tunahitaji kumuita mhudumu wa afya ili kusaidia.
 • TENGENEZA mchezo wa nyoka na ngazi ili kutusaidia kujifunza jinsi ya kukomesha kuharisha.
 • TENGENEZA Vifaa va Huduma ya Kwanza vya nyumbani na shuleni vilivyo na ORS.
 • IGIZA kuhusu akina mama wawili wakiongea kuhusu jinsi ya kuwasaidia watoto wao wanaoharisha kuwa vyema.
 • CHEZA mchezo wa kuonyesha picha ya mtoto anayeharisha ili kutambua kile tunajua kuhusu ishara za kupoteza maji mwilini.
 • ANGALIA jinsi mimea huhitaji maji ili kukua – chunguza ni nini hufanyika wakati mimea inakosa maji.
 • SAIDIA kuzuia kuharisha kwa kujiweka safi na kusafisha maeneo tunayoishi.
 • CHEZA Mchezo wa Kusalimiana ili kutambua jinsi ambavyo viini huenea kwa haraka.
 • WAULIZE wazazi wetu walinyonyeshwa kwa muda gani? Je, tunawezaje kutibu kuharisha kwa kutumia ORS na zinki tukiwa nyumbani? Je, ni ishara gani za hatari zinazoonyesha kuwa tunahitaji msaada kutoka kwa mhudumu wa afya? Ni vinywaji gani salama wakati tunaharisha? Je, tunawezaje kusafisha maji ya kunywa tukiwa nyumbani kwa kutumia jua? Ni vinywaji gani salama ikiwa hatuna ORS? Je, ugonjwa wa kuhara damu na kipindupindu ni nini na huenea vipi?

KKwa maelezo zaidi maalum kuhusu kutengeneza Mtego wa Nzi, Mchezo wa Kusalimiana au kuhusu kusafisha maji kwa kutumia jua au kitu kingine chochote, tafadhali wasiliana na www.childrenforhealth.org au clare@childrenforhealth.org
.

Swahili Home