Jumbe 100 za Afya kwa watoto za kujifunza & kushiriki ni rahisi, na ni jumbe za kuelimisha kuhusu afya zilizoaminika na zinalenga watoto wenye umri wa miaka 8-14. Hivyo hii inajumuisha vijana wenye umri wa miaka 10-14. Tuahisi kuwa ni muhimu sana na kuna manufaa kuhakikisha kuwa vijana wenye umri wa miaka 10-14 wanafahamishwa kwa sababu kundi hili mara nyingi hutunza watoto wadogo katika familia zao. Pia ni muhimu kutambua na kupongeza kazi wanayoifanya ili kusaidia familia zao kwa njia hii.

Ujumbe 100 unajumuisha jumbe 10 katika kila mojawapo ya mada muhimu ya afya: Malaria, Kuhara, Lishe bora, mafua na kukohoa, Minyoo, Maji na Usafi, Uchanjaji, Ukimwi, Ajali na Majeraha, Maendeleo ya Mapema ya Watoto. Ujumbe wa afya uliorahisishwa unalenga wazazi, waalimu wa afya ili kutumia kwa watoto nyumbani, shuleni, katika vilabu na kliniki.

Hizi ni jumbe 10 kuhusu mada ya 6: MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA

 1. Ili kuosha mikono vizuri, tumia maji na sabuni kidogo. Sugua kwa sekunde 10, kamua na kisha ukaushe hewani au kwa kutumia kitambaa au karatasi safi wala sio kwa nguo chafu.
 2. Osha mikono yako vizuri kabla ya kugusa eneo la T juu ya uso wako (macho, pua na kinywa), kwa sababu hapo ndipo virusi huingilia katika mwili. Epuka kugusa eneo linalotengeneza alama ya T jinsi unavyoweza.
 3. Nawa mikono KABLA ya kutayarisha chakula, kula au kuwapatia watoto chakula, na BAADA ya kuenda haja ndogo, haja kubwa au kusafisha mtoto au kumsaidia mtu aliye mgonjwa.
 4. Hakikisha mwili na nguo zako ni safi. Hakikisha kucha za mikono na miguu, meno na masikio, uso na nywele ni SAFI. Viatu/viatu vya kanda mbili huzuia minyoo.
 5. Hakikisha kuwa kinyesi cha binadamu na cha wanyama kimewekwa mbali na nzi ambao ndio hueneza vijidudu. Hakikisha kuwa unatumia vyoo na kisha kunawa mikono yako.
 6. Hakikisha uso wako ni safi. Osha vizuri kwa kutumia maji kidogo na sabuni kila asubuhi na jioni ikiwa nzi watapaa karibu na macho yenye uchafu.
 7. Usiguse maji safi na salama kwa mikono au vikombe chafu. Yaweke salama na kuyakinga dhidi ya vijidudu.
 8. Mwanga wa jua hufanya maji kuwa salama zaidi. Safisha kwa kutumia kichujio kwenye chupa za plastiki na uyawache kwa masaa 6 hadi yawe salama kunywa.
 9. Tumia jua kukausha na kuangamiza vijidudu kwenye sahani na vyombo baada ya kuziosha kila unavyoweza.
 10. Ua au upunguze wingi wa nzi kwa kuhakikisha nyumba na jamii yako haina taka na uchafu. Weka uchafu mahali salama hadi unapokusanywa, kuchomwa au kuzikwa

Jumbe hizi za afya zimeangaliwa na wataalamu wa elimu ya afya na wataalamu wa afya na pia zinaweza kupatikana kwenye tovuti ya ORB: http://www.health-orb.org.

Hii ni baadhi ya mifano ya mazoezi ambayo yatasaidida watoto kuelewa zaidi kuhusu mada na kushiriki ujumbe na wenzao.

MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA: Watoto wanaweza kufanya nini?

 • TENGENEZA ujumbe kuhusu MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA kwa kutumia maneno yetu wenyewe katika lugha yetu wenyewe!
 • KARIRI jumbe ili tusisahau!
 • SHIRIKI ujumbe pamoja na watoto wengine na familia zetu!
 • JIFUNZE wimbo utakaotusaidia kujifunza jinsi ya kuosha mikono.
 • TENGENEZA na IGIZA mchezo ili kuonyesha nini kinafanyikia Jamii ya viini wakati jamii safi inapohamia katika kijiji chao au igiza kuhusu mahali ambapo viini hupenda kujificha.
 • SAIDIA ndugu na dada zetu wadogo na uhakikishe kuwa wanajua jinsi ya kuosha mikono yao vizuri.
 • TUMIA muda wa saa moja kuangalia kundi la watu na utanzame na kurekodi ni mara ngapi wanagusa nyuso zao, nguo zao au watu wengine.
 • FIKIRIA njia zote ambazo viini vinaweza kuenea kutoka mikononi hadi mwilini.
 • SHIRIKIANA kutengeneza mpango wa kuhakikisha kwamba vyoo vya shule ni safi.
 • JIFUNZE jinsi ya kusafisha maji ukitumia kichujio.
 • FANYA mpango wa kuweka kiwanja cha shule safi na bila takataka.
 • ANZISHA klabu cha usafi wa mazingira shuleni
 • SHIRIKI kile tunachokijua kuhusu nzi, uchafu na viini pamoja na jamii zetu.
 • WEKA chombo chetu cha maji safi, kikiwa kimefunikwa na daima tumia chombo cha kuteka, na kamwe tusitumie kikombe au mikono yetu. Waonyeshe ndugu na dada zetu wadogo jinsi ya kuteka maji kutoka kwenye sufuria.
 • FANYA kazi pamoja ili kutengeneza – mfereji!
 • JINSI ya kutengeneza Taulo ishikilie sabuni ya kuosha miili yetu.
 • TENGENEZA Mtego wa nzi kutoka kwa chupa ya plastiki na maji ya sukari au kinyesi!
 • SAIDIA kutengeneza maji safi ya kunywa nyumbani Kwa kutumia Jua.
 • TENGENEZAKichujio cha Mchanga ili kusafisha maji chafu.
 • TENGENEZA ramani ya maji katika jamii yetu ili kujua ikiwa ni salama kuyanywa au la.
 • JENGA chanja ya kukausha sufuria za kupikia na sahani zetu ili ziweze kukauka chini ya jua.
 • ULIZA ni jinsi gani tunaweza kuweka mikono yetu safi na isiyo na viini? Je! Kuna sabuni ya kutumia kwa kuosha mikono nyumbani? Je, Bei ya sabuni katika duka za mitaa ni gani? Jinsi ya kuweka miili yetu safi? Jinsi ya kupiga meno yetu mswaki? Viini hutoka wapi, vinaishi wapi na ni jinsi gani vinaenea? Je, nzi huishi vipi, hula vipi na huzaana vipi? Je, nzi hubeba uchafu kwenye miguu yao vipi? Vyanzo vya maji yetu ni vipi? Tunawezaje kufanya maji chafu kuwa salama kunywa? Ni wapi tunaweza kupata chupa za plastiki? Je! Ni kitambaa gani kinachoweza kutumika kama kichujio cha maji? Je, ni utaratibu wa usafi mgani, ambao wanafamilia hutumia wakati wa kuandaa chakula? Ni wapi katika nyumba au jamii ambapo viini vinaweza kupatikana kwa wingi?

Kwa maelezo zaidi maalum kuhusu Mtego wa Nzi, Kutumia Jua ili kusafisha maji, jinsi ya kuunda Kichujio la mchanga, Taulo au Mfereji, au kitu kingine chochote, tafadhali wasiliana kupitia tovuti ya www.childrenforhealth.org au clare@childrenforhealth.org
.

Swahili Home