Jumbe 100 za Afya kwa watoto za kujifunza & kushiriki ni rahisi, na ni jumbe za kuelimisha kuhusu afya zilizoaminika na zinalenga watoto wenye umri wa miaka 8-14. Hivyo hii inajumuisha vijana wenye umri wa miaka 10-14. Tuahisi kuwa ni muhimu sana na kuna manufaa kuhakikisha kuwa vijana wenye umri wa miaka 10-14 wanafahamishwa kwa sababu kundi hili mara nyingi hutunza watoto wadogo katika familia zao. Pia ni muhimu kutambua na kupongeza kazi wanayoifanya ili kusaidia familia zao kwa njia hii.

Ujumbe 100 unajumuisha jumbe 10 katika kila mojawapo ya mada muhimu ya afya: Malaria, Kuhara, Lishe bora, mafua na kukohoa, Minyoo, Maji na Usafi, Uchanjaji, Ukimwi, Ajali na Majeraha, Maendeleo ya Mapema ya Watoto. Ujumbe wa afya uliorahisishwa unalenga wazazi, waalimu wa afya ili kutumia kwa watoto nyumbani, shuleni, katika vilabu na kliniki.

Hizi ni jumbe 10 katika mada ya 7: LISHE BORA

 1. Ili kuwa na chakula bora na cha afya kula vyakula tofauti vya aina tofauti. ENDA, KUA na ANGAZA ili kuwa na miili yenye nguvu na akili zenye furaha!
 2. Utapiamlo inamaanisha lishe mbaya na hutokea ikiwa tunakula chakula kidogo sana, kingi au zaidi tunakula vyakula visivyo na lishe ya kutosha. Epuka utapiamlo! Keti na ule chakula cha kutosha wakati wa chakula lakini sio kingi.
 3. Ili kuangalia kwamba watoto wachanga na watoto wadogo wanakua vizuri, angalia na saidia kurekodi urefu na uzito wao katika kliniki mara kwa mara na kama ilivyoagizwa na mfanyakazi wa afya.
 4. Saidia kuepuka madhara ya maisha kwa watoto wadogo. Waambie watu wazima wamuone daktari ikiwa utaona mikono au mwili unaonekana mwembamba au uso au miguu inaonekana kuvimba.
 5. Watoto wadogo wanapokuwa wagonjwa hawawezi kula vizuri. Wape vinywaji vyenye afya, kwa mfano maziwa ya mama, maziwa au supu iliyotengenezwa nyumbani. Pia, wape chakula cha ziada wakati wanaanza kuhisi vizuri.
 6. Kuwa bingwa wa maziwa ya mama! Maziwa ya mama daima ni safi na huwa ndio chakula PEKEE na kinywaji ambacho mtoto anahitaji kutoka kuzaliwa hadi miezi 6.
 7. Saidia kuandalia na kupea watoto wakubwa chakula bora (miezi 6 hadi miaka 2). Wanahitaji maziwa ya mama na chakula cha familia na vitafunio mara 3-4 kwa siku.
 8. Kula mchanganyiko wa matunda, mboga ikiwa ni pamoja na majani (nyekundu, machungwa ya njano na kijani). Zina virutubisho vidogo sana ambavyo si rahisi kuonekana lakini muhimu kwa mwili na akili zetu.
 9. Osha mikono yako vizuri kwa kutumia maji na sabuni kidogo. Papasa papasa kwa sekunde 20, suuza, tikisa na kausha kwa hewa baada ya kutumia choo na kabla ya kuandaa chakula na kula.
 10. Osha chakula safi unapokiandaa. Tumia chakula kilichopikwa mara moja au hakikisha kimehifadhiwa mbali na nzi ili kiwe salama kula baadaye.

Jumbe hizi za afya zimeangaliwa na wataalamu wa elimu ya afya na wataalamu wa afya na pia zinaweza kupatikana kwenye tovuti ya ORB: http://www.health-orb.org.

Hii ni baadhi ya mifano ya mazoezi ambayo yatasaidida watoto kuelewa zaidi kuhusu mada na kushiriki ujumbe na wenzao.

LISHE BORA: Watoto wanaweza kufanya nini?

 • PATA kifungua kinywa chenye afya kila siku.
 • KULA vyakula safi vya aina nyinyi ya rangi kila siku au kwa wiki.
 • AGIZA mayai zaidi, maharagwe na vyakula safi vya rangi kama matunda na mboga.
 • PATA vitafunio vya afya kama matunda au viazi vitamu.
 • NAWA mikono yako kwa kutumia sabuni baada ya kutumia choo na kabla ya kula na saidia watoto wadogo pia.
 • JIEPUSHE na vyakula vingi vya kukaanga, vinywaji vya sukari na vitafunio.
 • SAIDIA kwa ununuzi wa chakula na jifunze KUSOMA NA KUELEWA lebo za chakula.
 • JIFUNZE kuandaa na kupika vitafunio vyenye afya na chakula chenye afya.
 • JADILI ni chakula gani cha mitaani kina afya / kisicho na afya na ni kwa nini.
 • (na mtu mzima) TENGENEZA ujumbe wa LISHE BORA kwa kutumia maneno yako mwenyewe kwa lugha yako mwenyewe. KARIRI ujumbe wa lishe bora na USHIRIKI ujumbe na wengine wengi.
 • Unda HADITHI au MSURURU wa PICHA ZISIZO HALISI ili kukumbuka ujumbe wa lishe bora.
 • TAFUTA na UREKODI
  • Ni akina mama wagani katika jumuiya yako waliwanyonyesha watoto wao na ni kwa nini?
  • Je, maziwa ya mama hubadilikaje jinsi mtoto anavyokua?
  • Ni wakati upi chupa ni hatari kwa mtoto?
  • Akina mama huwapa watoto wao chakula kipi cha kwanza baada ya miezi 6?
  • Ni mara ngapi wananyonyesha katika umri tofauti?

  TENGENEZA chati na marafiki ili kuonyesha matokeo kwa wengine.

 • CHUNGUZA chati ya ukuaji wa mtoto mchanga na watu wazima ili kusaidia (hii mara nyingine huitwa Chati ya Barabara ya Afya).
 • TAFUTA maana ya mistari. TAZAMA watoto na watoto wachanga wakipimwa na uzito wao kupangwa kwenye chati yao.
 • TAFUTA & UREKODI
  • Je, familia yako hula nini kila siku / kila wiki?
  • Ni kiasi gani cha chakula cha familia kina rangi?
  • Je, kila mtu katika familia yako anapata aina mbalimbali za chakula ili KWENDA, KUKUA, NA KUNG’AA?
  • Je, kuna baadhi ya wanafamilia hasa wazee au hasa vijana ambao wanahitaji wengine KUZINGATIA na KUTOA MAONI juu ya kiasi kidogo ama kikubwa wanachokula?

  CHORA na ANDIKA kuhusu vyakula tunavyokula kila siku kwa wiki.

 • JADILI ikiwa kuna watoto wowote unaowajua ambao ni, au wanaweza kuwa, na utapiamlo na UPANGE, ni nini unaweza kufanya ili kuwasaidia.
 • ULIZA na USIKILIZE habari kuhusu wakati chakula kiliwafanya watu wawe wagonjwa (mfano chakula kilichohifadhiwa sana)
 • TAFUTA na uwe na mjadala juu ya mada kama:
  • Jinsi ya kutambua ikiwa mtoto anapatwa na utapiamlo
  • Ni vyakula vipi vilivyo na virutubisho vinavyopatikana kwa watu wengi katika jamii
  • Jinsi ya kuandaa mboga ili ziwe tamu
  • Kwa nini ni muhimu kula chakula chenye rangi cha kiasili
  • Ni vyakula gani vizuri kwa watu kula wakati wako wagonjwa na baadaye
  • Sababu gani na kwa nini, Matiti ni bora
  • Njia za kuweka chakula safi kama vile kukausha au kutumia chupa
  • Jinsi ya kutambua ikiwa chakula kimeharibika na hakifai tena kwa mlo
 • Jinsi ya kumsaidia mtoto aliye mgonjwa kupata chakula na vinywaji vizuri.
 • TANZAMA
  • Jinsi chakula huandaliwa & kupikwa
  • Jinsi sahani na vifaa vinavyooshwa na kukaushwa
  • Ikiwa mtu anayepika huosha mikono na sabuni kabla ya kugusa chakula.
 • CHORA chati ya picha inayoonyesha vyakula ambavyo havina afya kwa ajili ya watoto wachanga na watoto wadogo na UANDIKE karibu na kila picha kwa nini chakula hicho si cha afya. (k.m. sukari na kalori tupu).

Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na www.childrenforhealth.org au clare@childrenforhealth.org
.

Swahili Home