Jumbe 100 za Afya kwa watoto za kujifunza & kushiriki ni rahisi, na ni jumbe za kuelimisha kuhusu afya zilizoaminika na zinalenga watoto wenye umri wa miaka 8-14. Hivyo hii inajumuisha vijana wenye umri wa miaka 10-14. Tuahisi kuwa ni muhimu sana na kuna manufaa kuhakikisha kuwa vijana wenye umri wa miaka 10-14 wanafahamishwa kwa sababu kundi hili mara nyingi hutunza watoto wadogo katika familia zao. Pia ni muhimu kutambua na kupongeza kazi wanayoifanya ili kusaidia familia zao kwa njia hii.

Ujumbe 100 unajumuisha jumbe 10 katika kila mojawapo ya mada muhimu ya afya: Malaria, Kuhara, Lishe bora, mafua na kukohoa, Minyoo, Maji na Usafi, Uchanjaji, Ukimwi, Ajali na Majeraha, Maendeleo ya Mapema ya Watoto. Ujumbe wa afya uliorahisishwa unalenga wazazi, waalimu wa afya ili kutumia kwa watoto nyumbani, shuleni, katika vilabu na kliniki.

Hizi ni jumbe 10 kwenye mada ya 8: MINYOO

 1. Mamilioni ya watoto wana minyoo wanaoishi ndani ya miili yao, katika sehemu ya mwili inayoitwa matumbo na hapa ndipo ambapo chakula tunachokula hutumika na miili yetu.
 2. Aina tofauti za minyoo zinaweza kuishi katika miili yetu: mviringo, mjeledi, minyororo na bilharzia (schistosomiasis). Kuna nyingine pia!
 3. Minyoo inaweza kutufanya tujihisi wagonjwa ama wanyonge. Wanaweza kusababisha maumivu ya tumbo, kukohoa, homa na ugonjwa.
 4. Minyoo wanaishi ndani ya mwili wako hivyo huenda usiwe na ufahamu lakini kuna wakati mwingine unaweza kuona minyoo kwenye kinyesi chako.
 5. Minyoo na mayai yao huingia katika miili yetu kwa njia tofauti. Wengine huingia kupitia kwa chakula au kunywa maji yasiyo salama. Wengine huingia kupitia miguu peku.
 6. Kuua minyoo kwa kutumia dawa ni rahisi na nafuu. Zinapeanwa na wafanyakazi wa afya kila baada ya miezi 6 au 12, au zaidi kwa baadhi ya minyoo.
 7. Mayai ya minyoo huishi katika mkojo na kinyesi. Tumia vyoo au uondoe mkojo na kinyesi salama. Nawa mikono yako kwa kutumia sabuni baada ya kuenda haja ndogo ama kubwa au ikiwa umemsaidia mtu mwingine mdogo ili mayai ya minyoo isikushike kwa mikono.
 8. Zuia minyoo kuingia ndani ya mwili wako kwa kuosha mikono na sabuni baada ya kuenda haja ndogo ama kubwa na kabla ya kuandaa chakula, kula au kunywa, kwa kuosha matunda na mboga, na kwa kuvaa viatu.
 9. Minyoo wengine wanaishi katika udongo hivyo daima safisha mikono yako na sabuni baada ya kuugusa.
 10. Wakati wa kumwagilia mboga maji au matunda ya kula, tumia maji ambayo hayawezi kuwa na mkojo au kinyesi cha binadamu ndani yake.

Jumbe hizi za afya zimeangaliwa na wataalamu wa elimu ya afya na wataalamu wa afya na pia zinaweza kupatikana kwenye tovuti ya ORB: http://www.health-orb.org.

Hii ni baadhi ya mifano ya mazoezi ambayo yatasaidida watoto kuelewa zaidi kuhusu mada na kushiriki ujumbe na wenzao.

MINYOO: Watoto wanaweza kufanya nini?

 • TENGENEZA ujumbe wetu kuhusu minyoo kwa kutumia maneno yetu wenyewe katika lugha yetu wenyewe!
 • KARIRI jumbe ili tusisahau!
 • SHIRIKI ujumbe pamoja na watoto wengine na familia zetu!
 • TUMIA ‘piga kura kwa miguu yako’ kufanya jaribio letu na kujua ni kiasi gani unajua kuhusu minyoo.
 • SIKILIZA hadithi kuhusu minyoo ili tuweze kuelewa jinsi tunaweza kuzuia ueneaji wa minyoo kwa kuosha mikono yetu na kwa kukumbuka kuvalia viatu vyetu.
 • PATA KUFAHAMU jinsi chakula huandaliwa katika shule yetu na jinsi mpishi wetu anavyohifadhi chakula salama kutoka kwa minyoo.
 • Tumia choo au msalani DAIMA ili kuzuia kuenea kwa mayai ya minyoo yanayotokana na kinyesi ambacho huingia kwenye udongo na maji.
 • KUOSHA mikono yetu vizuri kunahitaji sabuni na maji na nguo safi.
 • FANYA utafiti ili kujua kile wanafamilia wetu wanachokijua kuhusu minyoo.
 • TENGENEZA mchezo wa kuigiza kuhusu minyoo wabaya na jinsi watoto huwazuia minyoo wabaya kutoiba chakula cha familia zao!
 • TENGENEZA mabango ili kuonyesha jinsi ya kuweka chakula salama bila minyoo kwa kuosha kabla ya kula mboga, kupika nyama vizuri na kuandaa chakula.
 • JUA jinsi ya kuunda mfereji na utengeneze Kituo cha Kuosha Mkono cha familia yetu, darasa letu au kikundi chetu.
 • TENGENEZA wimbo kuhusu jinsi ya kuzuia kuenea kwa minyoo au kuhusu kuosha mkono ili kutukumbusha wakati na jinsi ya kuosha mikono yetu.
 • TENGENEZA bango ili kutukumbusha kuosha mboga na matunda kabla ya kula au kuandaa.
 • IGIZA au TENGENEZA mchezo wa vikaragozi kuhusu jinsi ya kuzuia minyoo kuenea.
 • BUNI na IGIZA Mchezo wa maneno wa kujaza mapengo ili kupima ufahamu kuhusu minyoo, au BUNI na KUFANYA MTIHANI kujua wakati mwafaka wa kunawa mikono
kabla ya kufanya jambo and wakati mwafaka wa kunawa mikonobaada ya kufanya jambo. Tumia maswali yaliyo hapa chini ili kusaidia.
 • ULIZA jinsi miili yetu hutumia chakula tunachokila. Utumbo wetu mkubwa una urefu upi? Minyoo hupata chakula chetu vipi? Minyoo aina ya tapeworm inaweza kukua hadi kiwango cha urefu upi? Unajua aina ngapi za minyoo? Ni aina gani ya minyoo ni rahisi kupatikana unakoishi? Dalili za kuwa na minyoo ni zipi? Ni wapi unaweza kupata dawa za minyoo na ni nani anazihitaji? Minyoo wanaweza kutaga mayai mangapi kwa siku? Minyoo wanaweza kufyonza madini kama Vitamini A pamoja na chakula kutoka kwenye miili yetu – unaweza kutafuta ni kwa nini tunahitaji Vitamini A? Watoto wa minyoo wanaitwa mabuu. Ni aina gani ya mabuu huingia kwenye miili yetu kupitia kwenye ngozi? Kutumia choo na kutupa kinyesi chetu kwa njia salama kutatusaidiaje kuzuia kuenea kwa minyoo? Je, shule yetu imetenga siku za kutupatia dawa za minyoo? Ni siku gani? Kwa nini kila mmoja wetu hupata dawa za minyoo katika siku moja sawa? Ni watoto wangapi wana minyoo duniani? Kwa nini ni muhimu kuzuia minyoo kuenea? Kuhusu mfumo wetu wa kusaga chakula – unafanya kazi vipi na ni jinsi gani minyoo huuzuia kufanya kazi? Je, yai ya minyoo ni ndogo kiasi gani? Ni kitu kipi ambacho ni kidogo sana unachokijua? Tunaweza kujua vipi ikiwa maji ni safi au ni chafu? Mimea inahitaji nini ili kukua? Tunawezaje kutengeneza mbolea ambayo ni salama kwa kulisha mimea?

Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutengeneza mfereji au mahali pa kunawia mikono au Mchezo wa kujaza mapengo au chochote kile, tafadhali wasiliana kupitia tovuti www.childrenforhealth.org au clare@childrenforhealth.org
.

Swahili Home