Jumbe 100 za Afya kwa watoto za kujifunza & kushiriki ni rahisi, na ni jumbe za kuelimisha kuhusu afya zilizoaminika na zinalenga watoto wenye umri wa miaka 8-14. Hivyo hii inajumuisha vijana wenye umri wa miaka 10-14. Tuahisi kuwa ni muhimu sana na kuna manufaa kuhakikisha kuwa vijana wenye umri wa miaka 10-14 wanafahamishwa kwa sababu kundi hili mara nyingi hutunza watoto wadogo katika familia zao. Pia ni muhimu kutambua na kupongeza kazi wanayoifanya ili kusaidia familia zao kwa njia hii.

Ujumbe 100 unajumuisha jumbe 10 katika kila mojawapo ya mada muhimu ya afya: Malaria, Kuhara, Lishe bora, mafua na kukohoa, Minyoo, Maji na Usafi, Uchanjaji, Ukimwi, Ajali na Majeraha, Maendeleo ya Mapema ya Watoto. Ujumbe wa afya uliorahisishwa unalenga wazazi, waalimu wa afya ili kutumia kwa watoto nyumbani, shuleni, katika vilabu na kliniki.

Hizi ni jumbe 10 kwa mada ya 9: KUZUIA AJALI NA MAJERAHA

 1. Eneo la kupikia ni hatari kwa watoto. Waweke mbali na moto na vifaa vikali au vizito.
 2. Watoto wanafaa kuepuka kupumua moshi utokao kwenye moto. Husababisha ugonjwa na kukohoa.
 3. Kitu chochote chenye sumu ni lazima kihifadhiwe mbali na watoto. Usiweke sumu kwenye chupa za vinywaji.
 4. Ikiwa mtoto amechomeka, weka maji baridi kwenye eneo lililochomeka mara moja hadi uchungu upungue (dakika 10 au zaidi).
 5. Magari na baiskeli huua na kujeruhi watoto kila siku. Tahadhari kwa magari na uonyeshe wengine jinsi ya kuwa salama.
 6. Angalia hatari kwa watoto kama vile visu, glasi, nyaya za umeme, nyaya, misumari, pini na kadhalika.
 7. Zuia watoto kula uchafu, kuweka vitu vidogo ndani au karibu na midomo (kwa mfano sarafu, vifungo) kwa vile zinaweza kukaba koo.
 8. Zuia watoto kucheza karibu na maji ambapo wanaweza kuanguka ndani (mito, maziwa, vidimbwi, visima).
 9. Tengeza vifaa vya huduma ya kwanza nyumbani au shuleni (sabuni, makasi, dawa ya kuua viini, pamba, kipima joto, bendeji na ORS).
 10. Unapoenda mahali papya na mtoto, tahadhari! Angalia na kuuliza kuhusu hatari kwa watoto

Jumbe hizi za afya zimeangaliwa na wataalamu wa elimu ya afya na wataalamu wa afya na pia zinaweza kupatikana kwenye tovuti ya ORB: http://www.health-orb.org.

Hii ni baadhi ya mifano ya mazoezi ambayo yatasaidida watoto kuelewa zaidi kuhusu mada na kushiriki ujumbe na wenzao.

KUZUIA AJALI NA MAJERUHI: Watoto wanaweza kufanya nini?

 • TENGENEZA yetu wenyewe KUZUIA AJALI NA MAJERUHI ujumbe kwa kutumia maneno yetu wenyewe katika lugha yetu wenyewe!
 • KARIRI jumbe ili tusisahau!
 • SHIRIKI ujumbe na watoto wengine na familia zetu!
 • TENGENEZA mabango kuhusu kuweka sumu salama: jinsi ya kuzihifadhi, kuweka alama na kuziweka mbali na watoto.
 • TENGENEZA Kisanduku cha huduma ya kwanza tunachoweza kutumia ikiwa mmoja wetu amejeruhiwa.
 • TENGENEZA vifaa vya kuchezea ambavyo ni salama kwa watoto.
 • TENGENEZA kamba na kitu cha kuelea kinachoweza kutumika kwenye ziwa au mto wakati wa dharura.
 • TENGENEZA Kituo cha huduma ya kwanza cha shule yetu.
 • UNDA kampeni ya usalama ili kuongeza ufahamu wa kila mtu kuhusu usalama wa watoto.
 • FANYA utafiti kujua ni wapi kwenye jamii ambapo kuna maji yanayoweka watoto kwa hatari ya kuzama na ni nini kinachoweza kufanywa kuwaweka salama.
 • CHEZA lakini kwa nini? Mchezo kuhusu ajali nyumbani.
 • FIKIRI kuhusu njia za kufanya nyumbani kuwe salama na usambaze fikira hizi kwa mabango, nyimbo na michezo.
 • ULIZA kutoka kwa mhudumu wa afya ni nini kinahitajika kwa kisanduku cha huduma ya kwanza nyumbani na shuleni.
 • BUNI na KUCHEZA mchezo wa kutambua hatarikwenye bango au mchoro ili kuona ikiwa tunaweza kupata hatari zote.
 • ANZA kampeni ya kuhamasisha usalama wa watoto kwenye barabara.
 • IGIZA MCHEZO wa ufahamu wa usalama wakati tunapomtunza mtoto.
 • JIFUNZE huduma ya kwanza ili tuweze kusaidia katika dharura, igiza ili kuendeleza na kutekeleza ujuzi wetu wa kupatiana huduma ya kwanza na kuwashirikisha familia na marafiki zetu.
 • Angalia na kutambua hatari zozote kwa watoto nyumbani.
 • SHIRIKI yale tunayojua kuhusu hatari kwa watoto wadogo walio mikononi mwa watu wazima.
 • Jifunze cha kufanya wakati mtoto anabanwa kooni na kuonyesha wazazi wetu, akina babu na nyanya, kaka na dada.
 • JUA kutambua mahali kuna hatari ya kuchomeka, kuanguka, kuzama au barabara zenye magari mengi.
 • ULIZA hatari za kuchomeka zilizoko nyumbani. Tunafaa kufanya nini ikiwa mtu amechomeka? Tunawezaje kuwakinga watoto dhidi ya vitu moto na vioevu moto jikoni? Je, watu huweka watoto wachanga na watoto wadogo mbali na hatari katika jamii? – vipi? Ni kwa nini watoto wachanga wako kwenye hatari kubwa zaidi ya kunyongwa ikilinganishwa na watoto wenye umri mkubwa au watu wazima? Tunawezaje kumsaidia mtu aliye katika hatari ya kuzama bila kujiweka hatarini?

Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutengeneza mfereji au vifaa vya kuweka kwenye kisanduku cha huduma ya kwanza, au mfano wa bango la Kutambua Hatari, tafadhali wasiliana kwenye tovuti www.childrenforhealth.org au clare@childrenforhealth.org
.

Swahili Home