Our Messages in Swahili

Jumbe 100 za Afya kwa watoto za kujifunza & kushiriki ni rahisi, na ni jumbe za kuelimisha kuhusu afya zilizoaminika na zinalenga watoto wenye umri wa miaka 8-14. Hivyo hii inajumuisha vijana wenye umri wa miaka 10-14. Tuahisi kuwa ni muhimu sana na kuna manufaa kuhakikisha kuwa vijana wenye umri wa miaka 10-14 wanafahamishwa kwa sababu kundi hili mara nyingi hutunza watoto wadogo katika familia zao. Pia ni muhimu kutambua na kupongeza kazi wanayoifanya ili kusaidia familia zao kwa njia hii.

Ujumbe 100 unajumuisha jumbe 10 katika kila mojawapo ya mada muhimu ya afya: Malaria, Kuhara, Lishe bora, mafua na kukohoa, Minyoo, Maji na Usafi, Uchanjaji, Ukimwi, Ajali na Majeraha, Maendeleo ya Mapema ya Watoto. Ujumbe wa afya uliorahisishwa unalenga wazazi, waalimu wa afya ili kutumia kwa watoto nyumbani, shuleni, katika vilabu na kliniki.

Jumbe hizi za afya zimebuniwa na kuangaliwa na wataalamu wa elimu ya afya na wataalamu wa afya. Zinaweza kutafsiriwa na kutumika mradi ujumbe huo wa afya umesalia sahihi. Utunzaji mkubwa umefanyika ili kuhakikisha ujumbe wa afya ni sahihi na wa kisasa. Walimu wa afya hutumia ujumbe huu wa afya kuunda shughuli za elimu ya afya katika madarasa na miradi yao ili kuchochea majadiliano na shughuli zingine.

Kwa mfano, baada ya kusoma ujumbe kuhusu kunawa mikono kwa ubora, watoto wanaweza kuulizana au kuuliza familia zao Ni kwa nini watu katika familia na jamii yetu hushindwa kunawa mikono yao ifaavyo? Watoto huzungumzia jambo hili na kuamua kwa pamoja jinsi wanavyoweza kutatua tatizo hili na hivyo kuwa maajenti wa mabadiliko, ndio umuhimu wa kusoma ujumbe wa afya. Ujumbe huu ni kama mlango wa majadiliano na utekelezaji.

Wazazi na walimu wanaweza kuwauliza watoto wakariri ujumbe wa afya. Au, watoto wanaweza kuunda vitendo vinavyoambatana na kila ujumbe wa afya ili kuwasaidia kukariri ujumbe. Zawadi ndogo zinaweza kutuzwa watoto ambao wamesoma NA kushiriki ujumbe wa afya pamoja na wengine. Kwa mfano, nyuzi au kitambaa chenye rangi kinaweza kupeanwa kama zawadi. Watoto wanaweza kufunga kitambaa na nyuzi hizi kwenye kijiti na wafurahie kuunda kijiti chenye rangi nyingi ili kuonyesha ujumbe wa afya waliosoma na kuushiriki.

Ujumbe 100 wa Afya kwa watoto wa kujifunza & kushiriki umeundwa na Children for Health, shirika ndogo lisilo la serekali lililoko Cambridge huko UK. Children for Health hufanya kazi na washirika wa elimu ya afya kote duniani.

Ujumbe wa afya umeangaliwa na wataalamu wa elimu ya afya na wataalamu wa afya na pia unaweza kupatikana kwenye tovuti ya ORB: http://orbhealth.com.

  1. Kutunza watoto
  2. Kikohozi, mafua na ugonjwa
  3. Uchanjaji
  4. Malaria
  5. Kuhara
  6. Maji na usafi wa mazingira
  7. Lishe bora

  8. Minyoo
  9. Kuzuia ajali na majeraha
  10. HIV na UKIMWI